January 5 Tanzania iliandika historia mpya ya kibweka kilichotokea Shinyanga ambapo ndugu wa mwanamke mmoja
aliyefariki walimpasua tumbo marehemu huyo na umnyunyuzia damu yakifaranga kisha kumuwekea kifaranga cha
kuku kikiwa kizima.
Mashuhuda
wa tukio hilo wanasema kuwa marehemu alifariki akiwa na tatizo la
uvimbe tumboni, makubaliano yao ilikuwa kwamba wafanye shughuli hiyo
wakati mwili wa marehemu akiwa hospitali lakini mtafaruku ukazuka pale
ambapo ndugu hao waliamua kufanya zoezi hilo wakati jeneza limeshushwa
ndani ya kaburi.
Watu
waliamua kususia mazishi baada ya mtu huyo ambapo ndugu wakaamua
kufanya mazishi hayo wenyewe ambapo Polisi waliingilia kati pia kujua
chanzo cha mtafaruku huo.
Imesemekana
mzozo wa mazishi hayo ulitokana na kijana aliyemuoa mwanamke huyo
kutotoa mahari hivyo ndugu hao wakataka wapewe pesa kiasi cha mil.2 ili
waruhusu mazishi hayo yafanyike. Badala yake ndugu hao wa marehemu waliambulia shilingi laki moja tu!
No comments:
Post a Comment