WAKATI mwili wa mtuhumiwa wa dawa za kulevya, Abdul Koroma (33)
aliyeuawa wakati akijaribu kutoroka ukiendelea kuhifadhiwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa
Ilala limesema linasubiri kujitokeza kwa ndugu wa marehemu wakati wowote
kwa ajili ya kuja kuuchukua mwili huo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Mary
Nzuki alisema mbali ya kusubiri ndugu hao, pia wanasubiri utaratibu wa
ubalozi wa Sierra Leone, anapotokea marehemu huyo ili kujua nini hatua
zipi zichukuliwe na kwamba suala hilo lipo mikononi mwa polisi wa
kimataifa (Interpol).
Koroma aliuawa Desemba 31, mwaka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, alikopelekwa kusomewa mashitaka ya kukutwa na gramu 1,229 za
dawa za kulevya, zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Sh milioni 61
alizokamatwa nazo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Koroma aliuawa baada ya
kupigwa risasi na askari wakati akijaribu kuruka uzio kwa nia ya
kutoroka baada ya kuomba kwenda ‘kujisaidia’, tukio lililothibitishwa na
jeshi la polisi.
“Hadi ninavyozungumza hivi sasa, mwili wa marehemu bado unaendelea
kuhifadhiwa katika hospitali za Muhimbili, tukisubiri ndugu yeyote wa
marehemu kujitokeza au uamuzi wowote kutoka katika ubalozi wa nchi yake
kama wataamua asafirishwe au azikwe hapa hapa nchini,” alisema Nzuki.
Alisema kikubwa wanachosubiri kwa sasa ni taarifa za Interpol ili
kujua nini kifanyike kuhusu mwili huo kwa kuwa suala hilo hawawezi
kulimaliza hivi hivi kwa kuwa marehemu alikuwa raia wa nchi nyingine
tofauti na Tanzania.
Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey
Nzowa alisema kimsingi, kesi ya mtuhumiwa huyo kwa sasa imefutwa, kwani
mhusika hayupo tena duniani.
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Josephine is passionate, dedicated, reliable, responsible, and hardworking. Team worker and able to face all challenging situations. Can ...
No comments:
Post a Comment