Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa Migombani-Segera, Japhet Albert Kembo akiapishwa jana
jijini Dar es Salam.
- Wananchi wa Mtaa wa Migombani Segerea Wamwapisha Mwenyekiti wa Mtaa aliyeshinda pamoja na wajumbe wake
Tukio
hilo limetokea jana asubuhi katika ofisi za Serikali za Mitaa zilizopo
Segerea Mwisho ambalo lilijumuisha kuapishwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa
Migombani, Japhet Albert Kembo pamoja na wajumbe watatu ambao ni Rose
Benard Mhagama, Nyangeto Flora Justin na Ramadhan Rashid Seif.
Dar es Salaam. Baada
ya kusubiri kwa muda wa wiki mbili ili wajumbe serikali ya mtaa wa
Migombani-Segerea waapishwe na mamlaka husika bila mafanikio, wananchi
wameamua kuwaapisha viongozi hao kwa kutumia wakili binafsi.
Tukio hilo limetokea
jana asubuhi katika ofisi za Serikali za Mitaa zilizopo Segerea Mwisho
ambalo lilijumuisha kuapishwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa, Japhet Albert
Kembo pamoja na wajumbe watatu ambao ni Rose Benard Mhagama, Nyangeto
Flora Justin na Ramadhan Rashid Seif.
Akizungumza baada ya kuapishwa, mwenyekiti mpya wa mtaa huo amesema kuwa wananchi wamechoshwa na danadana wanazopigwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za kutowaapisha viongozi waliowachagua ndiyo maana wamefikia hatua hiyo ili kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
Akizungumza baada ya kuapishwa, mwenyekiti mpya wa mtaa huo amesema kuwa wananchi wamechoshwa na danadana wanazopigwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za kutowaapisha viongozi waliowachagua ndiyo maana wamefikia hatua hiyo ili kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
“Wananchi wanahitaji
huduma kutoka kwa watu wanaowaamini lakini wanakosa imani pale uongozi
wa manispaa unaposhindwa kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa kwa
mujibu wa sheria. Wamemtafuta wakili ambaye amekuja kulisimamia suala
hili kisheria na ndiyo maana zoezi limefanywa hadharani,” alisema Kembo.
Wananchi
waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa hawaelewi kinachoendelea
kwakuwa uchaguzi ulifanyika kama kawaida pasipo dosari yoyote na matokeo
yakatangwazwa huku nafasi zote zikichukuliwa na wagombea kutoka Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
“Uchaguzi wetu
haukuwa na matatizo na ni miongoni mwa mitaa iliyotangaza matokeo muda
mfupi baada ya uchaguzi kufanyika lakini jambo la kushangaza ni kwamba
viongozi wote waliochaguliwa hawajaapishwa kama ilivyofanyika kwa
wengine katika manispaa hii wakati hakuna pingamizi lolote mahakamani
linalozuia uhalali wa waliochaguliwa,” alisema John Kandeo, mmoja wa
wananchi walioshuhudia kuapishwa kwa viongozi hao.
Akifafanua kuhusu
matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 14, mwaka jana, Kembo alisema
kuwa walikuwa wagombea watatu katika nafasi ya uenyekiti ambao ni yeye
mwenyewe aliyepata jumla ya kura 547, Uyeka Idd wa CCM aliyepata kura
273 na Erick Mchata wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 205.
Zoezi lilivyokuwa
Muda wa saa 05:00
asubuhi, wakili wa kujitegemea kutoka kampuni ya mawakili ya Ame and
Company, Idd Msawanga aliwasili katika ofisi za mtaa huo na kupokelewa
kwa kelele nyingi za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipaza sauti zao kwa
sauti kubwa za ‘Peoples…Power.’
Wakili Msawanga
alianza kwa kumuapisha mwenyekiti, peke yake, na baadaye wajumbe hao
watatu kwa pamoja na kuelezwa kuwa wajumbe wawili hawakuwepo kutokana na
matatizo ya kifamilia.
“Sheria ya uchaguzi
inaruhusu kufanya hivi na hata hao wajumbe wawili ambao hawapo kwa leo
watakaporudi nitawaapisha…ni suala la kutaarifiana tu,” alisema
Msawanga.
No comments:
Post a Comment