Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange alipokuwa akimshukuru kwa kutoa vitabu kwa
Chuo cha Ulinzi na makataba zingine za JWTZ wakati wa hafla fupi ya
kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National
Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
Ijumaa January 9, 2015.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi baadhi ya vitabu na
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Rais Kikwete amekabidhi
vitabu hivyo 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National
Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa January 9, 2015. Rais kikwete, ambaye ameshachangia jumla ya
vitabu 2752 katika maktaba ya chuo hicho na maktaba zingine za JWTZ
katika vipindi tofati, amesema elimu imo vitabuni, na ili kuelemika
yapaswa mtu usome vitabu, na kwamba taasisi ya elimu inakamilika ikiwa
na vitabu.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis
Mwamunyange na maafisa waandamizi wa JWTZ wakiangalia vitabu wakati wa
hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha
Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es
salaam Ijumaa January 9, 2015.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhe Jacky Zoka, Balozi wa Tanzania
nchini Canada na Mhe Ali Siwa, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda,
walipofika Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa January 9, 2015 kuaga
rasmi kabla ya kwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi.
PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment