Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (katikati) alipoitishia mkutano na waandishi wa habari
jijini Mwanza mara baada kuhitimisha ziara zake Kanda ya ziwa. Kushoto
ni Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi
wa UN Tanzania, Bi. Chitralekha Massey.
Na Mwandishi wetu, Mwanza.
MRATIBU
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la maendeleo la Umoja huo, UNDP, Alvaro Rodriguez ameutaka uongozi mkoa
wa Mara kuanzia Polisi hadi serikali ya mkoa kuweka kipaumbele
kumtafuta binti albino ambaye ametekwa na watu wasiojulikana siku 14
zilizopita.
Hayo aliyasema jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini
Mwanza
baada ya kutembelea mkoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mara, Shinyanga na
Mwanza kuangalia miradi inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa pamoja na
masuala ya haki za binadamu.
Alisema
serikali kupitia Mkuu wa mkoa na Kamanda wa polisi mkoa wahakikishe
wanaendelea kumtafuta na kulipa suala la Pendo Emmanuel (4) kipaumbele .
Pendo
alitekwa na watu wasiojulikana baada ya mlango wa nyumba yao kuvunjwa
Desemba 27,2014 kwa jiwe la fatuma katika kijiji cha Ndami tarafa ya
Mwamashinda,wilayani Kwimba mkoani hapa ambapo hadi sasa bado
hajapatikana.
Aidha
aliwataka wananchi na viongozi kuhakikisha usalama wa watu wenye
ulemavu kwani wao ni binadamu kama binadamu wengine na wanahitaji haki
yao ya msingi ya kuishi bila hofu na manyanyaso kutoka kwa jamii
inayowazunguka. Mwakilishi huyo wa Umoja wa mataifa alisema katika
mkutano huo kwamba hata kurundikana kwa watoto walemavu wa ngozi katika
kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga ni matokeo ya mauaji
yanayoendeshwa dhidi yao na kusema suluhisho la tatizo hilo ni jamii
kuwakubali watu wenye ulemavu wa ngozi.
Tayari
watu 15 wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wa kuhusika na
uporwaji wa mtoto huyo akiwemo baba mzazi, Emmanuel Shilinde. Pamoja na
kuzungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza, kuelezea ziara yake
katika Ukanda wa Ziwa, Mwakilishi huyo pia alizuru wilaya ya Magu na
kukagua mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto
,UNICEF, wenye lengo la kuhakikisha haki inatetendeka dhidi ya wale
wanaonyanyasa watoto na haki zao za kibinadamu zinahesmiwa.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Akiwa
Magu alifurahishwa na mashikamano unaoneshwa na serikali na wadau
wengine kuhakikisha kwamba mradi huo unafanikiwa hasa katika kuwezesha
watu kutambua haki za msingi za watoto na kutoa msaada wa kisaikolojia
kwa watoto waliofanyiwa unyanyasaji na kuanzishwa kwa dawati la watoto
na jinsia vituo vya polisi. Hata hivyo aliambiwa changamoto
zinazoambatana na ukusanyaji wa taarifa hasa katika maeneo ya ndani
zaidi.
Katika
mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magese Mulongo, Umoja wa
Mataifa na Serikali ya Mkoa walikubaliana kwamba usalama wa wananchi
hasa watoto nay ale makundi maalumu ndio suala la msingi ambalo pande
zote hizo mbili itatilia maanani.
Akiwa
Shinyanga, Mwakilishi huyo Alvaro Rodriguez nalea kituo cha kulelea
watoto wenye ulemavu wa ngozi , wasiiona na viziwi Buhangija na kujionea
hali halisi ya mrundikano wa watoto. Kituo hicho kina watoto 220 wenye
ulemavu wa ngzoi ambao walikimbiziwa hapo baada ya usalama wao kuwa
shakani.
Alifurahishwa
na juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kuimarisha hali ya ustawi
katika kituo hicho ambacho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
zikiwemo za mrundikano wa watoto, afya na lishe.
Mkutano
na waandishi wa habari uliotishwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ukiendelea.
Alisema
akiwa hapo kwamba kama sehemu ya ajenda ya Umoja wa mataifa kusaidia
kulinda haki za binadamu na kuhakikisha wale wanaoishi na ulemavu wa
ngozi wanaendelea kustawi na haki zao zinaoheshimiwa, mwakilishi huyo
alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa msaada kwa kundi hilo.
Pia alifanya mazungumzo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na mkuu wa
wilaya hiyo Anna Rose ambapo walikubaliana kwamba suluhu ya mwisho ni
kwa watanzania kuwakubali wenye albinizim kama wenzao na kuacha
kuwatafuta kuwaua kwa imani za kishirikina. Akiwa mkoani Mara alishiriki
katika hafla ya kutunuku vyeti wasichana na wavulana waliofuzu mafunzo
ya miezi miwili yenye lengo la kuwaingiza katika jamii bila kukutwa au
kufanyiwa tohara yenye maumivu (kwa wavulana).
Mafunzo
hayo ni mchango wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la UNFPA wenye
lengo la kukabiliana na mila potofu ikiwamo ya ukeketaji na mimba za
utotoni zinazotokana na mabinti kuolewa wakiwa wadogo. Katika mazungumzo
na mkuu wa mkoa wa Mara, kapteni mstaafu Asery Msangi, Umoja huo
ulikubaliana na serikali ya mkoa kuendelea kushirikiana katika
kuhakikisha haki za msingi za binadamu zinaheshimika na wananchi
kuelimishwa kuhusu haki hizo.
No comments:
Post a Comment