JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatangazia Waheshimiwa
Wabunge wote, wadau na umma kwa ujumla kuwa Kamati za Kudumu za Bunge
zitaanza vikao vyake tarehe 13 hadi 23 Januari 2015. Vikao hivyo
vitakavyoutangulia mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge la Kumi vitajadili
na kuchambua pamoja na mambo mengine Miswada mbalimbali ya sheria.
Miswada itakayopitiwa na chambuliwa (pamoja na kamati husuka kwenye mabano) ni hii ifuatayo:
i. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014], [Kamati ya Mambo ya Nje]
ii. Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]
iii. Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa Mwaka 2014 [The Firearms and Ammunition Control Bill, 2014], [Kamati ya Ulinzi na Usalama]
iv. Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa Mwaka 2014 [The Disaster Management Bill, 2014], [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala]
v. Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa Mwaka 2014 [The Non-Citizen Employment Regulation Bill, 2014], [Kamati ya Maendeleo ya Jamii]
vi. Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa Mwaka 2014 [The Chemist Professionals Bill, 2014], [Kamati ya Huduma za Jamii]
vii. Muswada wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2014 [The Government Chemistry Laboratory Bill, 2014], [Kamati ya Huduma za Jamii]
viii. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Warehouse Receipts (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara]. Angalizo: Wakati wa uchambuzi Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara itashirikiana na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.
ix. Muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill, 2014], [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]
x. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscelaneous Amendments) Bill, 2014, [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala]. Angalizo: Aidha inashauriwa wakati wa kuchambua Muswada huu Kamati za kisekta zishirikishwe kwenye kutoa maoni kwenye marekebisho ya sheria ya sekta husika.
xi. Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014 [The Budget Bill, 2014], [Kamati ya Bajeti]
Aidha,
kwa taarifa hili Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wanaombwa kuwasili Jijini Dar es Salaam tarehe 12
Januari 2015 tayari kwa kuanza kazi tarehe 13 Januari 2015.
Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habri, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa
07 Januari, 2015.
No comments:
Post a Comment