Viongozi wa vyama vya siasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete
kutekeleza ahadi yake aliyoahidi wakati wa mkutano na wazee wa Dar es
Salaam ya kufanya maamuzi ya kumwajibisha waziri wa nishati na madini
ambaye alimweka kiporo na kudai kuwa atatoa maamuzi ndani ya siku mbili
lakini hadi leo amekaa kimya.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Iibrahim Lipumba amesema
suala la viongozi wakiwemo mawaziri kuwajibika halikuanza leo hasa
anaposhindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuisababishia
serikali hasara au kushusha heshima ya taifa hivyo ni vyema uwajibikaji
ukawa ni kwa kila mtumishi wa umma bila kubagua ili kuleta tija kwa
taifa.
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha
mapinduzi CCM Bw Najim Msenga amesema niimani ya chama chake kuwa rais
atafanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa kama alivyoahidi na kwamba
suala hilo haliwezi kuathiri uhai wa CCM kwani bado iko imara baada ya
baadhi ya watuhumiwa kuchukuliwa hatua.
Akizungumzia suala hilo katibu mkuu wa chama cha demokrasia na
maendeleo Chadema Dk Willbroad Silaa amesema hata hao waliojiuzulu na
kuenguliwa uteuzi wao maadam uchunguzi ulifanywa na vyombo sahihi hadi
kufikia hatua ya kupelekwa bungeni na kujadiliwa na wao kutoa maazimio
watuhumiwa wote hadi sasa walipaswa wawe wamefikishwa mahakamani.
Katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam uliofanyika ukumbi wa
Diamond Jublee desemba 22 mwaka jana Rais Kikwete alitengua uteuzi wa
aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh Anna
Tibaijuka na kutangaza kumweka kiporo waziri wa nishati na madini Prof
Muhongo.
No comments:
Post a Comment