17 January, 2015

YALIYOJIRI 'WATUHUMIWA WA ESCROW" MAHAKAMANI JANA


 MZIMU wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, limeendelea kuwatafuna watuhumiwa wa uchotwaji wa mabilioni ya fedha za akaunti hiyo baada ya watuhumiwa wengine watatu kupandishwa jana (16 Januari 2015) kizimbani katika mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
 Waliopandishwa ni Meneja wa Misamaha ya Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Leonard Mutabingwa ambaye anadaiwa kupokea rushwa ya zaidi ya shilingi bilioni moja kama zawadi kutoka kwa Rugemalira, Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Mkombozi , Julius Ruta, ambaye anadaiwa kupokea zaidi ya shilingi milioni 100 pamoja na Ofisa Mwandamizi wa Tanesco, Steven Urasa, anayetuhumiwa kupokea zaidi ya shilingi milioni 100.
 Mpaka chanzo cha habaru huu kinatoka mahakamani hapo ni mtuhumiwa mmoja tu aliyefanikiwa kuwa nje kwa dhamana ya kuweka nusu ya fedha anazotuhumiwa kupokea akitakiwa kuwa na watu wawili kama wadhamini. Watuhumiwa wengine walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi zao kutajwa tena tarehe 27, 29 Januari na 11 Februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...