27 April, 2015

MAMA MWENYE NYUMBA AKUTWA MTUPU CHUMBANI KWA MPANGAJI WAKE!

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Asha (pichani) mkazi wa Kitunda Masai, Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam wiki iliyopita alipata aibu kubwa baada ya kudaiwa kukutwa akiwa mtupu usiku katika chumba cha mpangaji wake.

Habari zinasema sakata hilo lilitokea wakati mama mmoja ajulikanaye kwa jina la Mama Bena alipoingia chumbani kwake baada ya kumsikia mwanaye wa miezi tisa akilia kwa sauti kali na alipofungua mlango alidai kumkuta mwanamke huyo chumbani karibu na kitanda alicholazwa mtoto wake.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zilisema kwamba, Mama Bena alipomkuta mama huyo chumbani kwake akiwa mtupu alimfungia mlango kwa nje akapiga mayowe na watu wakajazana huku wakiwa na mawe, mapanga na marungu wakaamuru mlango ufunguliwe ili wamuue lakini wasamaria wema wakatoa taarifa polisi ambao walifika
Habari zinadai baada ya polisi kufika, walilazimika kufyatua risasi ili kuweza kumchukua kwa usalama mwanamke huyo kutokana na watu wenye hasira kali kutaka kumpiga. “Polisi waliomba msaada wa wenzao ambao walifika na gari na kufanikiwa kumchukua mwanamke huyo ambaye alifunikwa shuka la mpangaji wake na kupelekwa Kituo cha Polisi Stakishari,” alisema shuhuda mmoja.


Baadhi ya polisi walithibitisha kufikishwa kituoni kwa mwanamke huyo, “Alijiharishia kituoni hapo wakati akiwa anahojiwa na polisi na hakujulikana mara moja ni kitu gani alichoenda kufuata katika chumba cha mpangaji wake huku akiwa uchi, sijui kama alikwenda kuwanga au alikuwa na nini,” kilisema chanzo cha habari hii

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...