Mshindi
huyo wa ‘Best Live Act’ kwenye MTV MAMA baada ya kurejea Tanzania,
amejibu shutuma alizozitoa Jojo dhidi yake kuhusu video aliyoipost, ya
mrembo huyo aliyewahi kuwa mpenzi wake akifurahia wimbo wa ‘Mdogo Mdogo’
na kuandika “Mbona Bado, Mtanyooka Tu”.
Kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm, haya ndio majibu ya Diamond kuhusu video aliyoipost na kile alichokiandika Jokate:
“unajua
kwanza nimecheka afu nimeskitishwa kwasababu nimeambiwa, sijasoma
nimeambiwa kuna post ameandika amezungumzia vitu vingi… Yeye kacheza
kama fan wa nyimbo yangu, na mimi nimempost kama fan wangu, ile caption
yangu sijamuandika jina kwanini achukulie vibaya? Ukiona mtu anajishuku
ukiona hivyo kuna namna nyuma. Mbona mi napost watu wengi tu, tena
naandika caption zangu za vituko vituko manake mimi nina caption za
vituko, mi ni mswahili nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale na Tandale
ndio kumenifanya leo niwe hapa nilipo…kwahiyo nina caption zangu za
uswahili kwasababu uswahili ndio umenikuza…siziachi kuziandika mbona
naziandikaga katika caption nyingi nyingi kwanini kwake yeye tu aione
tatizo, kwani kuna ubaya gani mi kuandika mtanyooka tu kama yeye
haimuhusu ina maana labda kuna kitu kinamuhusu.”
Diamond aliendelea:
“Nikaambiwa
pia amezungumza kwamba ndio maana wanaogopa kusapoti wasanii watanzania
kwasababu akisapoti wanadhalilishwa, yeye mimi mpaka nimeenda kuchukua
tuzo hii amenisapoti nini? Alipost hata post moja kusema mpigie kura
Diamond, afu leo anajishaua eti kanisapoti, kasapoti nini eti kutoa
hongera mi nimeshinda tuzo, eti ooh hongera kwa tuzo by the way,
angepost kuhamasisha watu wapige kura ili ushindi uje nyumbani, lakini
kwa chuki alizojazwa zisizo na sababu na roho mbaya alowekwa na watu
imemfanya ashindwe hata kunipost na kutengeneza chuki za chini chini kwa
kudhani wakiwapigia kura Wanigeria mi ntakosa tuzo…Mungu alivyolaani mi
nimeshinda, afu anajifanya anatoa hongera eti wanasapoti muziki wa
kiTanzania, utanisapoti nini, lini umenisapoti, au baada ya kuona tuzo
imekuja ndo unajifanya kutoa hongera, tuacheni unafiki.”
No comments:
Post a Comment