21 July, 2015

LOWASSA KUMSHITAKI KIKWETE!

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) alipokuwa anamnadi Edward Lowassa jimboni kwake Monduli 2010
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) alipokuwa anamnadi Edward Lowassa jimboni kwake Monduli 2010

The prime minister, who resigned, Edward Lowassa, has planned anytime from now, President Jakaya Kikwete kumkatia appeal.
The meeting between Lowassa and the media, targeting citizens to sue Kikwete for what he called, "defying the wishes of the majority."
 
Lowassa was among 38 members of the party were ripening in mbizo presidency, but his name was omitted in the initial stages. Kikwete was named kumuengua Lowassa for his personal interests.
WAZIRI mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amepanga wakati wowote kutoka sasa, kumkatia rufaa Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki zinasema, Lowassa amepanga kukutana na waandishi wa habari, Jumatatu au Jumanne wiki hii.

Mkutano kati ya Lowassa na vyombo vya habari, unalenga kumshitaki Kikwete kwa wananchi kwa kile kinachoitwa, “kukaidi matakwa ya wengi.”
Lowassa alikuwa miongoni mwa wanachama 38 wa chama hicho waliojitosa katika mbizo za urais, lakini jina lake liliondolewa katika hatua za awali. Kikwete ndiye anayetajwa kumuengua Lowassa kwa maslahi yake binafsi.
“Ni kweli kwamba Edo (Edward Lowassa), amepanga kueleza kilichotokea Dodoma kwenye mikutano ya chama chake. Atafanya hivyo kupitia mkutano kati yake na waandishi wa habari,” ameeleza mmoja wa watu waliokaribu na kiongozi huyo.
Hakuweza kufahamika mara moja, ikiwa Lowassa atautumia mkutano huo kueleza mustakabali wake wa baadaye wa kisiasa.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki, madiwani 20 kutoka jimboni kwake Monduli, walitangaza kukihama CCM na kujiunga na Chadema; jambo ambalo linadaiwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa ni maandalizi ya mwanasiasa huyo kukimbilia Chadema.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...