Msafara wa John Magufuli ukiwasili jijini Mwanza kwa ndege ya serikali
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kiko mbioni kufungua mashauri
mawili mahakamani dhidi ya John Pombe Magufuli, mgombea urais kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mabere Marando, mwanasheria mkuu wa chama hicho, kesi dhidi ya Magufuli itafunguliwa mahakama kuu, haraka iwezekanavyo.
“Tutamshitaki
Magufuli haraka iwezekanavyo. Huyu mtu ana sifa ya kutoheshimu utawala
wa sheria, hivyo tunataka kumuonyesha kuwa nchi hii inatawaliwa kwa
sheria,” anasema Marando kwa sauti ya ukali.
Anasema,
chama chake kitafungua mashauri mawili Shauri la kwanza litahusu
mwanasiasa huyo kuanza kampeni kabla ya wakati na jingine, ni juu ya
matumizi ya vyombo vya serikali kwenye kampeni za kisiasa.
“Yote
haya yatamhusu Magufuli na mawakala wake. Hatuwezi kuruhusu mtu mmoja
au chama kimoja, kinatumia madaraka yake binafsi na sisi tunanyamaza,”
ameeleza.
Marando
anasema, katika shauri la kwanza, chama chake kitawaunganisha
shirikisho la soka nchini (TFF); Baraza la Soka la Afrika Mashariki
(CECAF); CCM na wakala wa ndege za serikali.
Anasema,
TFF itaunganishwa katika shauri hilo kutokana na hatua yake ya
kumualika Magufuli kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano
yanayoandaliwa na CECAFA.
Hatua ya Chadema kuamua kufungua shauri dhidi ya mwanasiasa huyo imekuja baada ya MagufuliDar kutumia ndege ya Serikali katika anachoita, “kampeni yake ya kichama ya kujitambulisha.” wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa.
Magufuli, ametumia ndege ya serikali aina ya Fokker F28, alipokwenda Mwanza.
Lakini Nape Nnauye amesema, “…tumekodi ndege hii. Hatukupewa bure na yeyote anayetaka kuitumia aende kulipia tu, atapewa.”
Magufuli hakupatikana kueleza maoni yake juu ya hatua hiyo ya Chadema.
Katika
hatua nyingine, Marando amesema, mbali na kufungulia mashitaka
mahakamani dhidi ya Magufuli, CCM na mawakala wake, chama chake
kitawasilisha pingamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuomba kumzuia
Magufuli kuwa mgombea urais.
Anasema,
“tutamuwekea pingamizi kwa kuanza kampeni kabla ya wakati. Tunataka
tupate rais anayefuata sheria, siyo rais anayevunja sheria.”
Step Chadema decide to institute proceedings against the politician came after Magufuli Dar use of government aircraft in a call, "his campaign Organizational authentication." , saying the move was an abuse of public resources.
Magufuli, has used government aircraft types of Fokker F28, he went to Mwanza.
But Nape Nnauye said, "... we rent this plane. Hatukupewa free to anyone who wants to use it to go only to pay, will be given. "
Magufuli was not available to explain his views on that point of Chadema.
In
other action, Marando said, aside from prosecuting in court against
Magufuli, CCM and its agents, its members shall submit objections
National Electoral Commission (NEC), apply to dissuade Magufuli
presidential candidate.
He says, "we muwekea objection to begin a campaign before. We hope the president who follow the law, not the president who breaks the law. "
No comments:
Post a Comment