19 October, 2023

AKOSA ZAWADI YA GARI BAADA YA KUMTAJA MWANAUME TOFAUTI NA ALIYEMLETEA GARI HIYO AMBAYO ILIKUJA KAMA SUPRISE


Mwanadada huyo pichani kwa jina la Irene amejikuta akikosa zawadi ya gari Harrier new model (la thamani ya zaidi ya milioni 30) alilonunuliwa na mpenzi wake ambaye kabla ya kukabidhiwa ufunguo kupitia watu aliowatuma jamaa alimpa sharti amtaje jina kwanza ili ajue kama yuko peke yake. Matokeo yake mrembo huyo aliishia kujimumunya karibu dakika 10 asijue ni Mwanaume gani  amemtunuku zawadi hiyo kati ya mnyororo wa wanaume alionao na mwishowe alimtaja Mwanaume tofauti na aliyemletea zawadi hiyo.

 

Baada ya jamaa husika kupigiwa simu ili kujua jina alililotajwa kama ndo jina lake, Matokeo yake baada ya binti huyo kusikia sauti aliyoitaja siyo ya Mwanaume aliyekuwa amepigiwa, kwa aibu alikata simu akachukua virago vyake akatokomea kusikojulikana kuendelea na sherehe za graduation ya kuhitimu masomo ya chuo  kikuu cha Dar es salaam.

 

Katika mahojiano na Times Fm radio moja ya vijana walioshiriki kupeleka gari hilo amesema baada ya Irene kuondoka walimpigia simu jamaa na kumueleza akasema yeye haitwi BEN na hivyo akaagiza gari yake irudishwe. 

 

Katika mahojiano na leo tena ya Clouds Irene amejaribu kujitetea kwamba BEN alomtaja ni baba yake mzazi utetezi unaoonekana ni uongo mtupu inawezekanaje umtaje baba yako kama Boyfriend wako! 

 

Udangaji noma mabinti acheni tamaa

 

Wazoefu wa hizi kazi tunasema hii imeenda 😂

 

Endelea kutufuatilia....

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...