24 October, 2023

DIAMOND KASINGIZIWA MTOTO ALIE ZAA NA HAMISA??

 



Wiki hii Mwanamuziki Diamond Platnumz aliwachukua watoto wake Latiffah na Nillan ambao wanaishi kule Afrika Kusini kisha akawaleta Dar es salaam nyumbani kwake wakaungana na Naseeb Junior mtoto wa Diamond Platnumz na Tanasha. Watoto hao watatu wameonekana wakiponda raha za dunia, huku Diamond Platnumz na mama Dangote wakitia maneno ya hapa na pale kuonyesha jinsi wanavyowafurahia watoto hao.

 Hali hiyo imewakwaza mashabiki wanaomfatilia Diamond Platnumz ambapo kulingana na posti aliyoiposti mama Dangote, wengi wao wameonyesha kutamani kama Diamond angemchukua mtoto wa Hamissa Mobetto Dylan, ajumuike na watoto wenzake, lakini inaonekana wamemtenga na hawataki kusikia hata harufu yake.

 

Uzuri ni kwamba watu wengi wanachukizwa na hiki anachokifanya Diamond na wanamuombea mtoto wa Hamissa Mobetto ajaaliwe baraka na Mungu ili baadae Diamond aje kujutia anachomfanyia mtoto huyo, ingawa hakuna anayejua yanayoendelea nyuma ya Pazia.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...