10 August, 2016

RAIS MAGUFULI NI DIKTETA!!!








Kama Kweli ni Dicteta Basi Huu Ndiyo 'UDICTETA' wa Magufuli

🔰Kama Kupambana na Ufisadi nchini ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama kupunguza safari za nje zisizo na umuhimu ambazo zimelalamikiwa tangu awamu ya 4 ni Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama Rais Kutangaza mshahara wake ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama Kuhakikisha kuwa wabunge, Ma DC, Ma RC, nk wanakatwa kodi ya kiinua mgongo, nitamchagua tena 2020
🔰Kama kurejesha nidhamu ktk utumishi wa Umma ndiyo Udicteta,nitamchagua tena 2020
🔰Kama kuhakikisha kuwa madawa yanapatikana mahospitalini ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama Serikali kuhamia Dodoma ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama kuwaza kufufua viwanda ndiyo Udicteta,

nitamchagua tena 2020 
🔰Kama kutatua changamoto ya madawati nchini ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama Kupigania Elimu bure ndiyo Udikteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama Kubana Matumizi Ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama kufufua reli ya kati ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama kuwaza kukuza na kusapoti wajasiriamali wadogo ndiyo Udicteta, nitamchagua tena 2020
🔰Kama Rais kuwa mkali kuhusu maliasili na utajiri wa nchi hii ni Udicteta, nitamchagua tena 2020

Inaendelea................
👓 Mbingu zinajua na watanzania wanajua 👓
‪#‎My_Take‬ :Mwaka 2020 Watanzania watawahukumu wale wote wanaoyafanyia maisha ya watanzania maigizo

UTAFITI: KUNGURU MWITU WANAWEZA KUTENGENEZA ZANA

Wanasayansi wamethibitisha kwamba aina ya kunguru mwitu kutoka New Caledonia kusini mwa Pacific wanaweza kutengeneza zana.
Ndege hao walichunguzwa walipokua wakitumia midomo yao kuchukora chakula kilichokua kimefichwa kati kati ya mbao.
Awali ujuzi huu ullibainika kwa ndege wanaotunza kwenye maabara .
matokeo ya uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la Open Science, yanasema kuwa kipaji hiki ni sehemu ya tabia asilia ya ndege.
Mwaka 2002, kunguru mwitu anaetunzwa kwenye maabara ya New Caledonian crow - kwa jina Betty - aliwashangaza wanasayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Oxford walimpatia chakula katika kikapu kisichoweza kufikiwa kwa urahisi.
Kukifikia , ndege huyo alipindisha kipande cha waya hadi ndani ya kikapu. Ilikua ni mara ya kwanza kwa ujuzi huo wa kutengeneza kifaa kuwahi kushuhudiwa katika ulimwengu wa wanyama.
Betty alikufa mwaka 2005, lakini baada ya miaka, hatimae uchunguzi ulifanikiwa kurudiwa katika ndege mwingine alieko kwenye maabara.
Mkuu wa uchunguzi huo Dr Christian Rutz, kutoka chuo kikuu cha St Andrews cha Scotland, anasema : "ilionekana ni kama ni kitu ambacho ndege yule alikivumbua katika maabara ."
Wakati inafahamika kwa muda mrefu kwamba kunguru wa porini huweza kudonoa vitu kutoka kwenye sehemu zilizojificha za ndani , watafiti sasa wamebaini kuwa wanaweza pia kupindisha vijiti sawsa na wenzao wa maabara.
 
Kunguru 10 kati ya 18 waliweza kutengeneza vijiti vya kudonolea chakula
Katika msururu wa uchunguzi , watafiti waliwakamata kunguru kutoka misitu ya New Caledonia, na kuwaweka kwa muda mfupi katika viota vya muda
Dr Rutz anasema: "Hii inamaanisha kwamba tunaweza kuwafanyia majaribio katika hali ya uchunguzi unaodhibitiwa zaidi - lakini aina za vipimo tunavyofanya pale, havionyeshi vema namna ndege hawa walivuyo na akili , wanauliza ni aina gani ya kifaa ambacho wanakielezea kwa tabia asilia.
Kunguru walipewa vijiti , ambavyo vilikua na ladha ya chakula ambavyo viliwekwa kwenye mashimo kwenye sakafu
"Kitu kimoja tu tulichowapatia ulikua ni mmea ambao tulifahamu kwa kawaida wanatumia kutengenezea kifaa mwituni ," alieleza Dr Rutz.
"kwa hiyo kazi ilikua rahisi sana , tuliomnba ndege wetu watengeneze vifaa kisha tuvitumie kutoa chakula kilichofichwa ."
Kunguru hawakuhitaji vijiti maridadi kuchukua chakula , lakini 10 kati ya 18 wa mwituni walifanya hivyo.


Chanzo: BBC

UNAWAJUA MASTAA WASAGAJI BONGO?? LIST HII HAPA!!

MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Salmini ‘Sandra’ amewafungukia mastaa wenzake wenye tabia ya kusagana, sababu kubwa aliyoisema ya mastaa hao kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni kutopenda kuingia kwenye ndoa 

Sandra  alisema vitendo hivyo vimekuwa vikishamiri siku hadi siku kwa mastaa hususan wa filamu kwa tabia ya kupenda kuiga nchi za jirani, sababu nyingine aliyoiyaja Sandra ni kule kuchoshwa na tabia za wanaume wanaowatumia kimapenzi na kuwamwaga, pia kuogopa maambukizi ya magonjwa ya zinaa!!!

Usikae mbali na blog yako pendwa ya JoJoTheFighter kukuletea list ya mastaa wote wa bongo wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.





SIMU MILIONI 900 ZA ANDROID HATARINI!


Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani.
Upungufu huo unaowapa wadukuzi mlango wa nyuma wa kuiga herufi za siri uligunduliwa baada ya watafiti wa hali ya ubora wa programu Checkpoint walipojaribu kusuluhisha hitilafu iliyowezesha kirusi kuambukiza makumi ya mamilioni ya simu zilizokuwa na programu zilizoundwa na kampuni moja ya Marekani Qualcomm.
Kampuni hiyo inayounda programu za simu imeuza programu hiyo kwa watengenezaji wa simu milioni 900.
Hilo linamaanisha kuwa simu milioni 900 zipokatika hatari kubwa ya kudhibitiwa na wadukuzi.

Aina ya simu zilizoathirika

  • BlackBerry Priv na Dtek50
  • Blackphone 1 na Blackphone 2
  • Google Nexus 5X, Nexus 6 na Nexus 6P
  • HTC One, HTC M9 na HTC 10
  • LG G4, LG G5, na LG V10
  • New Moto X ya Motorola
  • OnePlus One, OnePlus 2 na OnePlus 3
  • Samsung Galaxy S7 na Samsung S7 Edge
  • Sony Xperia Z Ultra
Mkuu wa kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa programu katika kampuni ya Checkpoint Michael Shaulov, anasema kuwa
''hakuna ushahidi kuwa tayari simu hizo zimeathirika ila kwa mtizamo wetu ni kuwa mlango uko wazi kabisa mtu yeyote mwenye ufundi na ubora kama wangu hivi anafahamu waziwazi kuwa hakuna hata kizingiti cha kumuibia mtu herufi za siri katika simu hizo tulizotaja hapo juu''
Image copyright AP
Image caption Upungufu unamwezesha mtu wa tatu kumpokonya mmiliki wa simu udhibiti kwani anaweza hata akabadilisha herufi za siri bila yako wewe kujua.
''upungufu unamwezesha mtu wa tatu kumpokonya mmiliki wa simu udhibiti kwani anaweza hata akabadilisha herufi za siri bila yako wewe kujua''
''Ni hatari sana , ni kama mtu amejenga nyumba akaweka mle ndani mali ya thamani ya juu kisha akaondoka akiwa ameacha mlango wake wazi''alisema Shaulov.
Checkpoint tayari imeanza kutoa programu zenye uwezo wa kudhibiti simu hizo na tayari wameipa kampuni ya Qualcomm mbinu za kudhibiti simu hizo.
Njia moja ya kuimarisha usalama wa simu wanasema ni kununua programu kutoka kwa soko maalum la Google Play.
Qualcomm imenyamaza kimya kuhusu ripoti hii iliyotolewa na Checkpoint.

Chanzo: BBC

09 August, 2016

TUNDU LISSU AMEYASEMA HAYA LEO!!!

tundu lissuLeo mchana, Jumanee Agosti 9, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefnya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ili kutoa taarifa kwa umma kuhusu taarifa za vitisho wanazokuwa wakizipata kutoka serikalini.
Mwanasheria Mkuu wa wa chama hicho ambaye pia ni  Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe.  Tundu Antipas Lissu amesema hakuna mtu kutoka Chadema anayetaka kumjaribu mtukufu Rais na wala hakuna anayetaka kukamatwa na polisi  kwa sababu mahabusu sio pazuri.
“Tunachotaka kukifanya ni ambacho kipo katika katiba, mikutano na maandamano ya kisiasa kwakuwa ni halali. Kama kufanya hivyo Rais Magufuli anafikiri tunamjaribu hayo ni mawazo yake” Amesema Tundu Lissu.

ALICHOKIANDIKA DIAMOND PLATNUMZ SIKU YA BIRTHDAY YA MTOTO WAKE TIFFA

Kupitia mtandao wake wa Instagram Diamond Platnumz aliandika maneno haya kum'wish b day njema mtoto wake huyo wa kwanza, tiffa ama  Latipha Nasseeb Abdul

BIRTHDAY YA TIFFA YAWA GUMZO



Ana followers 623,049 Instagram, ni mtoto wa Diamond na Zari the Bosslady, unahitaji nini zaidi kukubali kuwa Tiffah ni supastaa mtoto kuliko wote Afrika?
Tayari mtoto huyo ana miezi 10 na hiyo ikimaanisha kuwa birthday yake ya mwaka mmoja inakaribia. Tiffah alizaliwa August 6, 2015.








UBUYU WA MJINI KUHUSU ZARI NA MOND


UNAFAHAMU KUHUSU HEKA HEKA ZA UKUTA SEPTEMBA 1?? SOMA HAPA.

1

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), limetangaza kuunga mkono operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta (Ukuta) iliyotangazwa hivi karibuni na Kamati Kuu ya chama hicho.

Aidha, Bavicha wamemjibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwamba hana mamlaka ya kuzuia operesheni hiyo kwa kuwa wanaifanya kisheria na yeye siyo msajili wa vyama vya siasa.

Makonda aliagiza Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya Ukuta, Ijumaa wakati akizungumza na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika kambi ya Ukonga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi, alisema maandalizi ya kuunga mkono operesheni hiyo yamekamilika kwa nchi nzima.

“Kauli ya Mkuu wa Mkoa (wa Dar es Salaam) ya kusema kwamba polisi wahakikishe Ukuta haujengeki, haitekelezeki kwa sababu yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo na wala si msajili wa vyama vya siasa hadi atoe kauli hiyo,” alisema Katambi.

“Zipo kesi nyingi zinazoonyesha wakuu wa mikoa kufanya kazi ambazo haziwahusu, hivyo kauli yake tutaipima kisheria,” alisema na kuongeza:

“Yeye akitaka aendelee kusema chochote akijisikia, lakini sisi tunamwambia kwamba mikutano yetu iko pale pale na tutaifanya nchi nzima.”

Katika mazungumzo yake na FFU, Makonda alisema askari wanafahamu sheria, hivyo wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo.

Aidha, aliwataka polisi hao kutosubiri maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais John Magufuli ameshaagiza kutofanyika kwa maandamano ya Ukuta yaliyopangwa kuwa Septemba mosi.

Makonda aliliagiza jeshi hilo kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwapo kitu kinaitwa Ukuta ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.

Lakini Mwenyekiti wa Bavicha jana alisema: “Tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ajiandae kutuma jeshi lake kulinda mikutano yetu.”

Kuhusu onyo la Rais Magufuli aliloitoa akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida kwamba Chadema isimjaribu kwa Ukuta, Katambi alisema chama hicho hakimjaribu.

Alisema Chadema itafanya maandamano nchi nzima kwa sababu kwa njia hiyo wanamsaidia kutoa mawazo yao kama vyama vya siasa kwa ajili ya kumsaidia kuendesha shughuli zake vizuri zaidi.

“Hatuna shida ya kumjaribu Rais, na wala si kwamba tunamchukia, na wala hatuna sababu ya kupinga uwapo wake, na hata ukiulizwa sasa kwamba Rais wako ni nani, lazima useme ni John Magufuli,” alisema Katambi.

“Tunapotoa dosari na kasoro tunamsaidia kuendesha nchi yake na watu walio chini yake.”

“Sisi kama vyama vya siasa tuna haki, tunajua yeye ndiye Rais, kama sisi hatukuweza kupata nafasi ya hiyo, haimaanishi kwamba ni vita, isipokuwa kupitia vyama vyetu, tuna sehemu ya kutoa mawazo yetu katika kuifanikishia serikali yake kuongoza vema pamoja na watu wake wa chini tena kwa mujibu wa sheria na inamsaidia yeye kuwa bora zaidi.
“Kwa hiyo kauli ya Rais sisi hatuna tatizo nayo.”

Katambi alisema taratibu zote za kisheria katika kutekeleza mikutano hiyo zitafuatwa.

Kamati Kuu ya chama hicho ilisema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini.

18 December, 2015

KOSA LA DR. MWAKA NI LIPI HASA??


Dr Juma Mwaka amefanya kosa gani Na Sheria inasema nini ?
Tangu Naibu Waziri wa Afya afanye ziara iliyoitwa ya kushtukiza katika kituo cha Foreplan Clinic kinachoendeshwa na Tabibu wa Tiba Mbadala Dr Juma Mwaka na taarifa kuenea kuwa Dr Mwaka alikimbia na wauguzi wake nao kutoweka, kumekuwa na mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii watu wakikinzana juu ya nini hasa kilichotokea.
Wako watu waliopongeza hatua ya Naibu Waziri na wako wengine wanaohoji juu ya kilichotokea. Jamii imegawika.
Binafsi nimefuatilia mijadala kadhaa na mwishoe nimeona niulize swali Dr Mwaka amefanya kosa gani?
Baadhi wamedai kosa lake ni kujiita Dr Mwaka, wakijenga hoja kuwa Dr ni mtu mwenye leseni ya kutibu, kufanya upasuaji, au tabibu wa meno n.k pia anakuwa na shahada katika kada hiyo.
Nimeshangaa hoja hiyo. Kama kila Dr lazima awe tabibu (medical practitioner) mbona kuna watu wengi wanaitwa ma-Dr ambao sio matabibu?
Kwenye kada ya sheria;
Dr Harrison Mwakyembe, Dr Tulia Akson, Dr Masumbuko Lamwai, Dr Cuthbeth Tenga n.k hawa ni ma Dr wa sheria lakini sio matabibu.

Kwenye kada ya Dini;
Dr Getrude Lwakatare, Dr Wibroard Slaa, Dr Alex Malasusa, Dr Sulley n.k hawa ni ma Dr wa dini lakini sio matabibu.

Kwenye kada ya Taaluma;
Dr Benson Bana, Dr Azaveli Lwaitama, Dr Abdallah Posi n.k hawa ni ma Dr lakini sio matabibu.

Kwenye kipengele cha Heshima;
Dr Reginald Mengi, Dr Jakaya Kikwete n.k hawa ni ma Dr wa Heshima (Honorary Doctorate) lakini sio matabibu.

Kwenye michezo ya kuigiza;
Dr Cheni sio tabibu.

Kwenye Tiba Mbadala;
Dr Matunge, Dr Rahabu Rubago, Dr Isaac Ndodi, Dr Sigwa, Dr Samson Kibona, Dr Manyaunyau, Dr Mwaka n.k hawa ni ma Dr wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala

Kosa la Dr Mwaka ni lipi?
Wako wanaosema kosa lake ni kujitangaza. Mbona ana vibali rasmi kujitangaza?
Nyaraka zake zinaonesha ameruhusiwa kufanya anachofanya.
SHIRIKA LA AFYA DUNIANI WHO LINASEMAJE KUHUSU SERA ZAKE KUFIKIA MWAKA 2039 KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA?
Moja ya sera ya shirika la afya duniani ni kuleta mahusiano makubwa katika tiba kati ya tiba asili na tiba ya kisasa yani modern medicine. Na hiki ndicho kilichofanyika China,india na mataifa mengine yaliyo endelea.
Unapokuwa china kuanzia ngazi ya dispensary kuna kitengo cha tiba asili na tiba mbdala hadi ngazi ya rufaa. Kwa kutekeleza hilo agiza Tanzania imeanza kwa kutengeneza TANZANIA INSTITUTE OF HERBAL MEDICINE ambayo inaendeshwa chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii katika chuo kikuu cha Muhimbili hadi sasa kuna Masters za herbal medicine. Sasa tunatakiwa kujua taifa au ulimwengu unaenda wapi, Tunahama kwenye kutibu kienyeji kwa ramli,matunguli, na unga ambao hauna kiwango tunasafiri kutoka kwenye LOCAL TRADITIONAL MEDICINE TUNAENDA KWENYE MODERN TRADITIONAL MEDICINES. Nchi kama china hadi sasa dawa za TRADITIONAL CHINESE MEDICINES ndio ngumzo katika soko zinazodhoofisha soko la viwanda vingi vinavyo tengeneza dawa za kemikali.
Kutokana na sera na mbio za mabadiriko hayo, na sera moja wapo ni kuacha kuhangaika kutibu dalili za magonjwa na kuanza kutibu chanzo kuanzia kwenye seli na viini lishe ndani ya seli. Hivyo ndio vifaa vya uchunguzi km vyakutumia compyuter ambavyo wenzetu kule hata family physician [Dakatri wa nyumba kumi ulaya] wanatumia kuangalia homoni zako,micronutrients,macronutrients nk. Sasa kwa nini Dr mwaka akitumia mnashangaa? Kuna mashine siku hizi ambazo zinatumika katika kutibu magonjwa mbalimbali, km msongo wa mawazo,maumivu ya misuli,kukosa usingizi, nk kupitia Thermal therapy, huwa nakutana na madakatri wenzangu wanavipinga! Huwa nacheka sana unapinga kitu ambacho kimefanyiwa dafiti na mtu mwenye elimu kukuzidi na kimeruhusiwa kutumia kidunia, wewe unapinga kwa kutumia mgongo wa udakatri na sio nyalaka na tafiti za kisomi kama kweli wewe ni dakatri na umefuzu vizuri ‪#‎FANYA‬ TAFITI KUHUSU VIPIMO NA TIBA HIZO UTULETEE DATA ZAKE ! Hapo ndipo utamgundua msomi na mvivu,mwenye chuki na asiyependa maendeleo ya wengine kila siku majungu. HEBU TUWEKE ELIMU PEMBENI KILA MTU AFANYE KAZI YAKE KATIKA NAFASI YAKE.

Moja ya sera ya kusajili madakatri wa Tiba asili wote ilikuwa na kuwatambua wote na kile kibali kinaonesha kabisa kama una Meno au ngozi au kitu chochote cha mnyama hakikisha unakisajili. Na hicho kibali kinazuia kubaini magonjwa kwa njia ya RAMLI.
Sasa Swali Mlitaka Dr mwaka apige Ramli ndipo ajue kuna Fibroids au Ovarian Cysts au PID?
Ndio maana taifa linaenda kwenye MODERN TRADITIONAL MEDICINES, Na endapo wataalamu wa afya msipo kubaliana na hili mtaaanguka kabisa na mtapotea kama vyama vya siasa vinavyopotea.
Hivi Mwaka anashindwa nini kusaidiana na wasomi wa Picha za mionzi Radiologists na hatimaye mwaka kupata jibu sahihi amtibu vipi mgonjwa? Tatizo Wataalamu wa afya wengi maisha ni magumu, na Walifikiria kusoma udaktari basi maisha yamenyooka, bado ni omba omba na hadi sasa hawezi hata kulipia kipindi cha ITV Unazani atakula nini kama vipindi kwa mwezi ni zaidi ya milion 3? Mshahara wake hapo Anakusanya miezi 2.
Kwa nini TUWE NA USHABIKI USIOKUWA NA MAANA YOYOTE?

Tatizo siwezi kuwa laumu sana baadhi ya watalaamu wa afya maana Mitaala yetu inatunyima uwanja wa kufikiri sana kwa sababu hizi;
-Unasoma shule kwa kutumia Mtaala wa chuo kikuu wa kuchukua Doctor of medicine.
-Unamaliza unawaza kuajiliwa tu, huwazi hata kutumia elimu yako kufanya tafiti nyingi kututatulia hizi sintofahamu sio kukaa unahangaika kutype kitu ambacho kinakurudisha nyuma kimaendeleo kwa kumwengea mtu ambaye amekuzidi chochote ulicho nacho hapo ulipo. FANYENI TAFITI WASOMI MANENO HATUTAKI KABISA MSOMI ONGEA KWA TAFITI SIO KUTUMIA UBAVU WA ELIMU YA MIAKA 7 AU KUMI.

-Ukimaliza chuo unatukiwa Doctor of Medicine degree unakutana na Guidelines yani hizi ni miongozo ya matibabu ya kimataifa na taifa.
Kuna Tanzania Treatment Guidelines na WHO Treatment guidelines. Hii miongozi inatufanya tuwe watu wakukalili tu bila kuwaza vitu vikubwa, Our mind is locked in the guideline. Yani yeye akisha kalili guideline ya kutibu malaria basi ameshakuwa Dr. Milele na milele.

Sasa Hebu akili zetu tuzitumikishe kabisa maana najua Future ya Dr mwaka ni kubwa sana kwa sababu hata hiki cheti mnachokiona ni mwaka mmoja kinaweza kuwa ni thamani kubwa kuzidi matarajio yenu.
Siku moja nilikuwa najaribu kuchambua kwa nini CHINESE TRADITIONAL MEDICINES NI MOST RANKED MEDICINES IN THE WORLD AND FIRST CLASS HERBAL MEDICINES? Kile kitabu kimenifumbua mengi na nimeshangazwa na kazi kubwa Dr mwaka aliyo ifanya kusomea mimea ya nchini china na tafiti za mimea ya china jinsi gani zinatibu magonjwa tabia.

"Tiba ya kisasa ina nafasi yake katika kutibu magonjwa, lakini pia tiba ya asili ina nafasi yake kubwa mno"
TATIZO TANZANIA TUNAPUNGUKIWA NA TAFITI KUHUSU TIBA ASILI NA WASOMI WENGI WANAIBEZA NA KUISHUSHA HADHI BILA KUJUA KUWA DAWA NYINGI ZINATOKA HUKO.

Watu wanasema Dr mwaka anawachunguza watu sehemu za siri! Huku hana elimu ya kumchunguza mgonjwa!
Hata Dakatri hatusomei kumchunguza mgonjwa sehemu za siri. Na ndio maana daktari hata kama wewe ni profesa ukamchunguza mgonjwa sehemu za siri bila ridhaa yake utakuwa umekiuka misingi ya udaktari. Sasa kuchunguzwa huko ni ridhaa kati ya Dakatri na mgonjwa usikubali kwa kinyongo kisa yeye ni dakatri hapana kama una nafsi ya kukataa kataa kabisa.
Sasa Hivi hawa wanaochunguzwa hawakutoa lidhaa? Kama hawakutoa ridhaa mbona hawakwenda kushitaki? Yani mimi nashindwa kuelewa watu tunawazia wapi.

Unakutana na mtu anasema Wanawapotezea wagonjwa Muda wanakuja Wamezidiwa.
Hivi mara ngapi mgonjwa wa kisukari,presha,uvimbe anahudhuria hospital bila mafanikio? Tena kila akija Dawa zinaongezwa na pesa juu ya kumwona daktari bingwa wa magonjwa hayo. Je mtu kwenda kwa Mwaka kujaribu kupata matibabu yake kuna kosa gani km huku ameshindwa kupona? Kwani afya ni Ridhaa ya Dakatri au yangu? Mimi ndio mwenye ridhaa ya afya yangu!
Mara ngapi unaposema wagonjwa hawaponi wanawaibia pesa, Hivi mara ngapi wagonjwa hawaponi hadi wengine hospitali wanachukua dama! Kwani mbona kila hospitali ina chumba cha maiti? Kwani Dr Mwaka Mungu kila mtu apone jamani? Duuu, huwa nasema modern medicines Dr wangekuwa kwenye taifa la waelewa wangeishia pabaya, maana wanataka wao wanachokifikiria tu ndio kiwe chema cha mwingine kiwe kibaya.
TIBA ASILI NA TIBA MBADALA UKILINGANISHA NA TIBA YA KIZUNGU NI PAKA NA PANYA.
Unaposema Mwaka ni Biashara tu, basi sema Dawa hizo za hospitali ziwe bure kabisa na kusiwepo na pesa ya kumwona daktari tuone kma kuna baadhi ya watumishi wa afya wataishi hapa duniani.
Wengine wanasema Gharama kubwa za matibabu kwa Dr mwaka anawaibia.
Nakupa Zoezi dogo tu kama msomi na mwelevu, Eating Organic is Expensive, Jaribu kula vyakula vya asili, matunda km blue berries, strawberries,cranberries,bittermelon,watermelon nk ,mboga za majani kma broccoli,caulifolwer, Celery nk utaona gharama kwa mwezi shilingi ngapi! Tuone kama utamudu na kamshahara hako, ndio maana watu wanaishia kula Chapati, wali,viazi,juisi ya 1000 soda ya 500 na kuishia kupata magonjwa ambayo yanawagarimu maisha.
Unaposema ni gharama jiulize swali ukiambiwa kula vyakula asili utaweza gharama?
Basi ndio maana ni gharama maana mengine matunda na mbegu zake upataiakanji ni shida sana.
SIO MUDA WAKUIBEZA TENA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA, KINACHOTAKIWA NI KILA MTU AFANYE KAZI KATIKA NAFASI YAKE NA KUTIMIZA MAJUKUMU.
TIBA YA KISASA NA TIBA MBADALA ZOTE ZIPO KIBIASHARA MAANA HAKUNA HUDUMA INAYOTOLEWA BURE KATIKA KILA IDARA HIZO MBILI.
Utofauti mkubwa katika tiba asili na tiba ya kisasa ni DAWA ZINAZOTUMIKA KUTIBIA MGONJWA.
Mfano: Daktari wa kisasa amebobea kutibu kwa dawa za kisasa ambazo zinamtaka Anayetumia kitiba awe amesomea na anaujua mwili wa binadamu vizuri.
Daktari wa tiba asili, yeye amebobea katika mimea yake na anaujuzi wa kina kujua hii dawa yangu ninapo mpatia mgonjwa inaenda kutibu kitu gani na inafanyaje kazi mwilini? Ndio maana watu wanagundua dawa za asili, kama ginsen herb tablets,Gingko biloba tablets, Cordceps sinensis capsules hizo ni baadhi ya dawa asili zinazokamata headlines hata ktk ulimwengu soma medscape na Rejea zingine sio kusoma vitabu vya mitaala tu mnakuja kutoa maneno ya wivu yanaonesha kabisa maneno ya mshindwaji.

Sasa unapokuja kusema Daktari wa tiba asili asichambue mwili wa binadamu kama aliusomea ina maanisha huna imani na dawa zake! Maana atatumiaje dawa ambazo yeye hajui zinafanya kazi kivipi ktk mwili wa binadamu? Inasikitisha tunashindwa kuwaza haya.
Tafiti za tiba asili zipo na zinaendelea na kama Dr mwaka ni Tabibu anaruhusiwa kuendesha tafiti za kisayansi na akagundua dawa.

Tunacho angalia ni uwezo wa kuwafikia watu wengi na kuwasaidia wengi.
Kosa la Dr Mwaka ni lipi? Ambalo linamuhusu yeye peke yake na haliwahusu wenzake wa Tiba mbadala?
Tizo Mwangosi Ujumbe mzur dia but mi najua kosa ni kukimbia kituo kwa dokta! Labda nambie pia km ni kwel alikimbia, kwann alkimbia!???
Mcrose Mbaga
Mcrose Mbaga Kwann atoke nduki?waziri ni muongo?
Gift Kangele
Gift Kangele hapa ndugu nianze kukushangaa maana ww ni kati waliofanya mjadala juzi na pia ipo hivi kuna kuna Dr yaan mtu mwenye shahada moja ya utabibu wa binadamu mf Doctor of Medicine na pia kuna Dr yaan mpaka usome shahada tatu ndipo utunukiwe hiyo mtu anakuwa mbobezi ktk jambo fulani yaan Doctorate of Philosophy(PhD) nadhani kwa kifupi umeelewa na hao wengne uliwataja wanaposses PhD.
Oliver Kassim Kassim
Shabanij Shabani
Shabanij Shabani Naomba kujibiwa swali,kwanini alikimbia...hilo ndio tatizo si angebaki ofisini na kupeana maelezo yahusuyo taaluma yake.
Gift Kangele
Gift Kangele Pia wala hakuna anayebeza tiba asili kuna taratibu zake kisheria moja ni kutafuta kibali maana kuna Baraza la Tiba asili la Taifa na pia dawa unatumia inabidi zikachunguzwe kwa mkemia mkuu wa serikali na wakiona zinafaa ndipo wakusajili na kukupa kiba...See More
Imma Sabuni
Imma Sabuni Siku ya mkasa wa Dr.Mwaka Josephine Joseph ulipost kicheko, nuliduwaa...ila nashukuru leo umekuja kurekebisha makosa yako with Vivid Details.
Manyumila Manota
Manyumila Manota Josephine Joseph kunakiwango cha kusoma ukikifikia ndio una ukawa dr katika traditional healer kama ngapi za certification, diploma, adv, Mpaka degree nakuendelea; lakini Zippo aina nyingi za kuna traditional healer kama vile kulisi ktoka kwa wazazi...... n. k.
Kanyika Lusato
Kanyika Lusato Nimeshangaa hoja yako kuhusu mtu kujiita Dr. Ni Kama huelewi unachoandika. Dr. Siyo Tu anayetibu sawa, lakini kuitwa Dr yoyote Kuna taratibu zake. Mimi Kama sina PhD halafu nikajiita Dr. Ili nipate kazi ya Lecturer Hilo Ni kosa. Kosa halipo kwenye kuji...See More
Hans A Chambasi
Hans A Chambasi Kanyika LusatoMtoa mada hajafanya utafiti vizuri.. Kaandika tu.. Ni vema kabla ya ku post kitu kufanya utafiti
George Ntalula
George Ntalula Vipindi vyake Dr Mwaka vina muda mrefu sana tena vipo karibu media zote za kielektronic na vingine, vyote hivi vinapatikana kwa watu wote hadi wa serikali, huo unaosemwa "ulaghai" umeonekana Jana?
Dokt huyu kasaidia watu wengi kadiri tunavyowaona
...See More
Mzazi Ronald
Mzazi Ronald Sheria ya matibabu huruhusiwi kujitangaza
Josephine Joseph
Write a reply...

Charles Tumaini
Charles Tumaini Mbona kila MTU mpaka Waziri wanamuita Dr Mwaka
Mzazi Ronald
Mzazi Ronald Miiko ya udaktari ni kuto jitangaza
Amos Ikwabe
Amos Ikwabe Tatizo ni lipi maana hata mm celewi maana kujiita Dr ni wengi wanajiita ila kama anasaidia hana tatizo afanye yake kinachotakiwa ni watu wapone tu.
Davydavidavy Davis
Ibrahim Christopher Shirima
Adam Bura
Adam Bura kumbe na wewe ni mbovu wa Ku reason kiasi hichi? unatetea upuuzi? yaani we umesoma mass comm ati kwa kuwa unajua panadol inatuliza maumivu basi ujiite Dr tena uliyebobea? huo ni ukilaza wa hali ya juu, mpaka hapo ulipo hujui Tofauti ya PhD ( Doctor of Philosophy) na Doctor of Medicine, ni ujasiri wa kipumbavu kutetea upuuzi eti hujasomea urubani halafu ujiite Rubani??? Hajasomea USS halafu eti anafanya USS na we mtanzania unasema yes, Yeye anageendelea na miti shamba take bila kuchanganya na modern medicine, pili hakuna sheria inayoruhusu kujisifu ama kujitangaza kuwa ni ninaweza hiki na kile, kumbe wanahabari kama wewe mpo chini ya kiwango kwa kuonesha akili ndogo kama hii, labda useme hii page yako ilkua manipulated
Josephine Joseph
Write a comment...

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...