08 June, 2012

TAARIFA: MKUTANO WA JANGWANI KESHO

NIMEIPATA HII KULE JAMII FORUMS. ATAKAYEVAA SARE YA CCM KESHO HAPANDI DALADALA - MAKONDA. Soma hapa.

Chama cha makonda mkoa wa Dar-es-Salaam (CHACHAMADA) na baadhi ya wamiliki wa mabus hayo ya usafiri ndani ya jiji la Dar wamekutana leo alfajiri somewhere (secret meeting) na kwa pamoja wameridhia kuwa kesho siku ya Jumamosi mtu yeyote atakayevaa vazi (nguo) lolote linaloashiria sare ya CCM (kijani au njano) hataruhusiwa kupanda dala dala yoyote....zoezi hili litaanza kesho kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa mbili usiku. Baada ya muda huo wataruhusiwa kuvaa nguo yenye rangi yeyote na ruksa kupanda daladala yeyote.

Angalizo: Sio watu wengi wanaoingia na kutumia mitandao. So ikopi hii message kama inavyojieleza kwa kutumia simu yako ya mkononi na uwatumie ndugu na marafiki zako wote wanaoishi ndani ya Dar na wanategemea usafiri wa mabasi (Dala dala).

Source - mtu anaemiliki daladala 5 zenye route tofauti hapa Bongo...

1 comment:

  1. Kumzuia mtu asipande daladala ambayo ni mojawapo ya huduma ya msingi kwa mtu wa DSM eti kwa sababu ana nguo au sare ya chama fulani cha siasa ni kupingana na kukiuka katiba ya nchi inayompatia kila mtu haki ya kuwa huru kwa nyanja zote ili mradi tu havunji sheria. Sijaelewa hili litafanyika kwa kutimiza sheria ipi au sehemu ipi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Naomba nieleweshwe. Mimi pia ni mwana harakati lakini hii haijanifanya nisimame juu ya sheria.

    ReplyDelete

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...