Majambazi
saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya
I&M jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa
kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika
makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda
wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa
Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa
tukio lenyewe ingawa mpaka sasa ni kama milioni zaidi 150
zinahisiwa kuibiwa.
Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa
katika eneo hilo amesema matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi
kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga upya.
Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki
hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili T220 AMV
na kuondoka nao kwa ajili ya mahojiano zaidi
Chanzo: Usawazi

No comments:
Post a Comment