Katika
kuonyesha amechoshwa na upweke, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
ameibuka na kusema kuwa sasa anasaka mwanaume wa kumuoa huku akitaja
vigezo vya anayestahili kumuita mume.
Akizungumzia
maisha yake ya kimapenzi, Jokate alisema kuwa hana ‘mtu’ ila
atakapotokea mwenye vigezo anavyotaka, hatakuwa na sababu ya kumkataa.
“Kwa sasa sina mpenzi wala mchumba, akitokea sina kipingamizi ila mbali
na vigezo vingine awe na mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Jokate.
Jokate amekuwa msiri sana katika maisha yake ya kimapenzi kiasi cha wengi kuamini ni msichana anayejiheshimu sana ila aliwahi kuwa na uhusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayekipiga kwenye Timu ya Oklahoma City Thunder ya nchini Marekani na Mwimbaji wa Bongo Flava, Diamond Platnumz.
No comments:
Post a Comment