05 August, 2014

KIJANA MMOJA AFA AKIJARIBU KUFUKUA KABURI ILI AIBE FUVU LA MAREHEMU

Maiti ya kijana huyo ikiwa imenasa kaburini
Tukio la ajabu na la kushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya kijana mmoja kukutwa kaburini akiwa amekufa huku kichwa chake kikiwa kimezama ndani ya kaburi hilo!
 Kijana huyo ambaye jina lake halijafahamika, alikumbwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi yanayodaiwa kuwa ya kishirikina.
Kwa mujibu wa mtandao wa Saturday Tribune wa Nigeria, tukio hilo lilitokea katika mji wa Ilobu eneo la Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa amefuatana na wenzake waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa pamoja, lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi, walikimbia na kumuacha akihangaika kujinasua. Hata hivyo, jitihada za kijana huyo kujinasua pale ziligonga mwamba na hivyo kupoteza maisha.

Hapa inaonekana miili miwili ya watu waliokufa ukiwemo aliyefia ndani ya kaburi, lakini hakuna maelezo juu yake
Mtandao wa Saturday Tribune ulibaatika kuongea na Kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilipelekea kijana huyo kupoteza maisha.

Msemaji wa jeshi hilo aliongeza kuwa mpaka sasa jeshi lake bado halijathibisha kwamba tukio hilo liliambatana na mambo ya   kishirikina kama inavyodaiwa na wakazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...