Mwendesha mashitaka anayejulikana kama Gerrie Nel ameitaka mahakama iliyokuwa inasikiliza kesi ya Pistorius kumuongezea adhabu kwa kile anachodai hukumu aliyopewa ni ndogo sana.
Jaji huyo Thokozile Masipa, aliahirisha kesi hiyo hadi siku ya Jumatano, akisema anataka muda zaidi kuchunguza tetesi zilizowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka ukitaka mahakama imuongfeze adhabu Pistorius.
Oscar Pistorius huenda akaachiliwa huru kutoka gerezani baada ya miezi kumi tu huku akitarajiwa kutumikia kifungo kilichosalia nyumbani.
Pistorius alifungwa jela miaka mitano mwezi oktoba kwa kosa la mauaji bila ya kukusudia na siku ya Jumatano mwendesha mashitaka atafahamu ikiwa anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Pistorius.

No comments:
Post a Comment