Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeifikisha mahakamani
Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kufuatia malalamiko ya wagombea wa
uchaguzi wa serikali za mitaa wa Chama hicho kuondolewa kwa tuhuma za
kutumia mihuri ya jina la chama hicho kwa ufupi pasipo na ufafanuzi.
Hayo yamezungumzwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa kitengo cha
habari wa chama hicho Tumani Makene nakusema kuwa maamuzi ya kuifikisha
TAMISEMI Mahakamani yameafikiwa kufuatia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kuwakilisha muongozo wa uchaguzi wa
serikali za mitaa bila kufanya marekebisho hali inayopelekea kuonekana
kupuuzwa kwa uchaguzi huo.
Ameongeza kuwa Wakati wanasheria na viongozi wa
CHADEMA kutoka maeneo mbalimbali Nchini wakiendelea na taratibu za
kisheria mahakamani ili kuhakikisaha haki inatendeka katika uchaguzi wa
serikali za mitaa unaendeshwa kidemokrasia ni vyema ofisi ya
TAMISEMI ikajipanga kurekebisha utaratibu wa muongozo wa uchaguzi huo.
Katika hatua nyingine Makene ameeleza kuwa endapo uchaguzi wa
serikali za mitaa utavunjika kwa kukosa haki za kidemokrasia na
kusababisha damu ya mtanzania ikamwagika ni wazi Mheshimiwa Pinda na
Ofisi yake itahusishwa.
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaanza vikao vyake tena leo mjini Dodoma, huku kukiwa na jitihada kubwa za kujaribu kuweka udh...

No comments:
Post a Comment