09 December, 2014

MUGABE AMTIMUA MAKAMU WA RAIS


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Joyce Munjuru.
Joyce Munjuru.
Rais Robert Mugabe amemfuta kazi makamu wake Joice Mujuru, kufuatia ushindani wa uongozi katika chama tawala cha ZANU-PF.
Awali Bi Joyce Mujuru, anadaiwa  kuwa yeye kuwa ni fisadi  pamoja na kuhusika na njama ya kutaka kumuua rais Robert Mugabe.
Bi Mujuru alilaaniwa na Rais Mugabe wiki iliyopita na kuondolewa kutoka wadhifa wake wa makamu wa rais wa chama tawala cha ZANU-PF wakati wa kongamano la chama hicho mjini Harare.
Kwa  upande  wake Bi Munjuru   amesema ameendelea kupokea vitisho na kuwa shirika la habari la serikali limeendelea  kuchapisha habari za uongo za zisizo na msingi dhidi yake.
Katika hatua nyingine  ilikuwa wiki nzima ya tuhuma dhidi ya Bi Mujuru kutoka kwa vyombo vya habari vya serikali kwa ushirikiano na mke wa  Mugabe, Grace Mugabe, ambaye kwa sasa ameteuliwa kama afisaa mkuu wa chama cha ZANU-PF

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...