20 January, 2015

"WEMA NIACHIE BOB JUNIOR WANGU"

Hapa na Pale:‘Wema Aniachie Bob Junior Wangu'
UBUYU! Siku chache baada ya kuripotiwa kwa tukio la staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kunaswa kimalovee na Rais wa Masharobaro, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, mwigizaji chipukizi, Bozi ameibuka na kudai ‘Wema niachie Bob Junior wangu’.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii, mara baada ya habari hiyo kuruka hewani kupitia gazeti moja wiki iliyopita, mrembo huyo alipoziona picha za wawili hao alipoteza fahamu.
Akizungumza huku akiangua kilio, Bozi alisema kuwa katika siku alizowahi kuumia ni siku hiyo alipoona Wema ametoka kwenye gazeti na mpenzi wake huyo.
Bozi alifunguka kwamba, alimbana Bob Junior kwa maswali lakini jamaa huyo hakutaka kumweka wazi kama yeye na Wema wanatoka.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...