01 December, 2023

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?


Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu


Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

 

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

 

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

 

Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

 

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

 

So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

 

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.

 

Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.

 

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

 

Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI".

                                             













 

18 November, 2023

AFISA WA POLISI WA TANZANIA ALIKODI RAFIKI ILI AMPE MKE WAKE MIMBA, AMFIKISHA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUMPA MIMBA BAADA YA KUJARARIBU MARA 77

Jijini Dar-es-Salaam, Mahakama ya Tanzania lazima iamue juu ya nia ya heshima katika kesi ambapo mwanamume alimwajiri jirani yake ili kumpa ujauzito mkewe.

 

Inaonekana kwamba Darius Makambako 50 akiwa na mke wake Precious 45, walitaka sana kupata mtoto, lakini daktari bingwa alikuwa amewaambia wanandoa hao kuwa mume alikuwa TASA. Hakukuwa na shaka, wenzi hao walikuwa wamechoka kuwa katika ndoa ya miaka 23 bila mtoto.

 

Kwa hiyo Makambako, askari wa Jeshi la Polisi (Idara ya Trafiki), baada ya kushurutishwa na mkewe, aliajiri jirani yake Evans Mastano, 52, afisa mwenza wa polisi katika jiji la kibiashara la Dar-es-Salaam kumpa ujauzito mke wake.

 

Kwa kuwa Evans alikuwa tayari ameoa na ni baba wa mabinti wawili warembo, na pia kwamba alifanana sana na Darius kindakindaki, mpango huo ulionekana kuwa mzuri kwa wanandoa hao wa familia mbili lakini bila kumshirikisha mke wa Evans.

 

Makambako alimlipa Mastano Shilingi 2,000,000 za Kitanzania kwa kazi hiyo ambayo angeshiriki tendo la ndoa na mkewe kwa jioni tatu kwa wiki kwa miezi 10 ijayo ya 2016.

 

Evans alijaribu sana, jumla ya mara 77 kumpa ujauzito mke wa rafiki yake Precious, lakini alishindwa kabisa kufanikiwa.

 

Ripoti zinasema Precious, ambaye kikazi ni muuguzi katika zahanati ya kibinafsi aliamua kuchukua likizo ya miezi mitatu (Machi hadi Juni 2016) ili kutenga muda wake wa kulala na rafiki mkubwa wa mumewe na jirani ili kupata mtoto wake wa kwanza, lakini mwanamume huyo alishindwa kumpa mimba licha ya mume kuwaacha kitandani siku nzima mara nyingi.

 

Na Precious aliposhindwa kupata ujauzito kwa miezi 10, hata hivyo, Makambako hakuelewa na kusisitiza kwamba Evans afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu, ambao alifanya Januari 2017.

 

Uchunguzi wa daktari

Ulionyesha kwamba Evans Mastano pia alikuwa TASA matokeo ambayo yalimshtua kila mtu isipokuwa mkewe (Evans), ambaye alilazimika kukiri kwamba Evans hakuwa baba halisi wa watoto wake wawili, bali walikuwa wa binamu yake, Edward.

 

" _Nililazimika kulala kwa siri na Edward, binamu yake wa kwanza, kupata watoto hawa wawili baada ya kugundua kuwa mume wangu hangeweza kunipa ujauzito kwa miaka miwili",_ Angela aliambia _Dar-es-Salaam Today News._

 

Sasa Makamboko anamshtaki Evans kwa ukiukwaji wa masharti ya mkataba katika jitihada za kurejesha pesa zake, lakini Evans anakataa kwa sababu alisema hakumhakikishia kupata mimba, lakini tu kwamba aliahidi kujitahidi na angefanya juhudi za uaminifu.

 

 *SWALI* : 

 

1. Je. Makambako ana haki ya kudai arudishiwe pesa yake? 

2. Nini itakuwa hatma ya ndoa kati ya Evans na mkewe Anjela?

 

Chanzo: *DAR-ES-SALAAM LEO.*


16 November, 2023

USHOGA SASA RUKSA!!

Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa. 

Wakati huo huo papa Francis amemfuta kazi askofu Joseph Strickland, ambae ni mkosoaji mkubwa alieibua maswali juu ya uongozi wa papa katika Kanisa Katoliki.

Askofu Srickland ni mmoja kati ya sauti kinara katika tawi la uongozi wa Kanisa Katoliki nchini Marekani ambalo linapinga vikali mabadiliko yanayopigiwa chapuo na papa Francis.

Kuondolewa kwakwe kunakuja baada ya papa kuzungumzia juu ya hali ya kuwa nyuma kifikra.



Chanzo: BBC News Swahili

15 November, 2023

JoJo The Fighter: JOJO THE FIGHTER BIOGRAPHY

JoJo The Fighter: JOJO THE FIGHTER BIOGRAPHY:    Josephine is passionate, dedicated, reliable, responsible, and hardworking. Team worker and able to face all challenging situations. Can ...

14 November, 2023

LADY JAYDEE AMLETEA ZAWADI MTALAKA WAKE

 

Staa wa Bongofleva, Lady Jaydee amemletea zawadi ya perfume mtalaka wake, Gardner G Habash ambaye ni Mtangazaji wa Clouds FM. 

 

Utakumbuka Lady Jaydee na Gardner walifunga ndoa Mei 2005 na kuachana rasmi kwa talaka Desemba 2016, ikiwa ni miaka 10 ya ndoa.

 

Je, wewe unaweza kumpa zawadi mtalaka au ex wako?.


SINA MUME, SINA MCHUMBA

 


⚠️😳 "Mume sina na mchumba sina, labda wananiogopa maana hatokei mtu wa kuniambia ananipenda nahisi wananiogopa, sijaolewa na mtu akija why not?"

 "Nataka kubadili dini nitoke kwenye ukristo niwe muislam, na sitabadili kwasababu ya mwanaume, ni mimi mwenyewe nimeamua kwasababu napenda mambo ya kiislamu"

 Aidha amesema "kufua sijui na hii itakuwa ngumu kidogo kwangu kwasababu dada yupo ananifulia, lakini pia kuna mashine za kufulia ila kupika niko vizuri kiasi" - amesema  Madame Rita

 Hata hivyo, Madame Rita amesema kipindi cha nyuma alishawahi kuwa katika mahusiano pia ana mtoto mmoja ila kwasasa ndio hayupo katika mahusiano na akitokea mtu wakapendana na kutaka kufunga ndoa hana hiana kufanya hivyo


PAPA FRANCIS NA NDOA ZA JINSIA MOJA

th

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja  si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Ingawa Francis alikosoa kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja, aliweka wazi kuwa anaamini kuwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni dhambi. "Hebu tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu," Papa alisema.


Chanzo: BBC

NAFANYA MAANDAMANO KUANZIA AIRPORT

 


Msanii wa Muziki kutoka Tanzania, Harmonize ambaye kwasasa yupo USA ameweka wazi kuwa ataanya paledi (Maandamano) kuanzia Airport mpaka konde Village,

 

"Tangu muziki wetu au niseme SANAA yetu ianze, SIKUMBUKI lini mara ya mwisho msanii kutoka Tanzania kulipatia hili Taifa la mama samia tuzo Tatu (3) za kimataifa ndani ya usiku mmoilja.! Moja au mbili, Nakumbuka ila Tatu sina kumbukumbu kwahiyo paledi litaanzia airport mpaka KONDE VILLAGE alafu tunakesha mpaka asubuhi, soon nawarudia na Tarehe pamoja na saa ninayotua ...! KONDE GANG MUDA WENU WA KUTAMBA.." ameandika Harmonize

 

 


13 November, 2023

JOJO THE FIGHTER'S CURRENT MOOD

 NEVER TRY TO DEFEAT THE UN DEFEATABLE. Its like to wound what you cannot kill. You shall definitely face the consequences. Its high time now to let the devil face what he deserves!









UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...