...yanasababisha sonona (depression)
Watafiti wa University of Pittsburgh School of Medicine walifanya
utafiti kuhusu madhara ya matumizi ya mitandao ya kijamii katika mood
ya watumiaji.
Utafiti huo ulibaini kuwa kadri vijana wanavyotumia mitandao hiyo zaidi,
ndivyo wanavyopata tatizo la sonona ambalo kitaalam linajulikana kama
depression, au kukosa uchangamfu na furaha.
“Kwasababu mitandao ya kijamii imekuwa kitu kilichojiweka kwenye
mawasiliano ya binadamu, ni muhimu kwa wauguzi kuongea na vijana kuhusu
kutambua uwiano unaotakiwa kuwepo na kuhimiza matumizi chanya wakati
wakijiondoa kwenye matumizi yenye matatizo,” alisema Brian A. Primack,
M.D., Ph.D., ambaye ni mwandishi mkuu wa utafiti huo.
Utafiti huo ulihusisha watu 1,787 nchini Marekani wa kuanzia miaka 19
hadi 32. Mitandao iliyohusishwa ni pamoja na Facebook, YouTube, Twitter,
Google Plus, Instagram, Snapchat, Reddit, Tumblr, Pinterest, Vine na
LinkedIn.
Washiriki walitumia mitandao hiyo kwa dakika 61 na kutembelea akaunti
mbalimbali za mitandao ya kijamii mara 30 kwa wiki, kiwastani. Cha
kutisha kwenye utafiti huo, zaidi ya robo ya washiriki walielezewa kuwa
na viashirio vya juu vya sonona.
Kulikuwepo na uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya mitandao ya kijamii na sonona.
Watafiti hao lakini walizitaja sababu zingine zinazochangia tatizo hilo
kuwa ni pamoja na umri, jinsia, rangi, uhusiano, hali ya maisha, kiwango
cha elimu na kipato.